Kauli ya Jaguar Baada Ya Kupokezwa Ushindi

Wanasiasa kwa kauli ya msanii Jaguar ni matapeli.Hii ni baada ya
msanii huyo kuibuka mshindi katika siasa za mchujo wa chama cha jubilee eneo la starehe.

Jaguar anaeleza kuwa kwa maeneo yote 27 ya kupigia kura ya starehe alikuwa anaongoza kwa vituo 25 vya kupigia kura.Ila mpinzani wake wa karibu,mbunge wa sasa Maina Kamanda,alitumia mbinu zote chafu kushida.

Maina Kamanda alijiongezea kura katika vituo viwili vilivyosalia.Pia alihusika pakubwa kwa mambo maovu kama kuzima stima.Jaguar alikuwa amekisia haya.Msanii huyo alikuwa amejipanga na taa.

»»  Zile Vitu Remix by Kenrazy and Avril

Baada ya kura zake kuibiwa,ilibidi Jaguar amwone rais ambaye ni mkuu wa chama cha jubilee.
Mrudio wakuhesabu kura ulianza na kisha akaibuka Mshindi.
image

“Wafuasi wangu walilia tulipoibiwa kura zetu.Nikitoa machozi si ya uwoga ila kupigania haki yangu.”Hii ndiyo iliyokuwa kauli ya Msanii Jaguar.

Kwa sasa Maina Kamanda amekubaliana na hayo matokeo na kuamua kumuunga mkono Msanii Jaguar.

Facebook Comments
About Dex Antikua 126 Articles
||Radio Presenter||Pro-Blogger||